Makamo rais wa kitengo hicho Shekhe Aadil Wakiil ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa “Mwezi wa Muharam na Safari inaumaalum wake katika kitengo chetu, ni miezi ya huzuni na kuomboleza, miezi ya kujikumbusha misingi ya harakati ya Imamu Hussein (a.s) katika mapambano yake ya milele, yaliyo angaza dunia nzima katika kila zama na mahala”.
Akaongeza kuwa: “Kitengo chetu kinafanya kazi mwaka mzima, lakini katika miezi hii miwili huwa tunafanya kazi zaidi, huongeza ratiba ya utendaji kwa ajili ya kunufaika na msimu huu, kufuatia umaalum wa kuhudumia mazuwaru na jamii kwa ujumla, miongoni mwa mambo tunayo fanya ni:
- - Kuratibu mihadhara tofauti ya uombolezaji ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
- - Kufanya vikao vya kutoa mawaidha na maelekezo kwa mazuwaru karibu na muda wa swala ya Dhuhuraini, kwa kueleza misingi na malengo ya harakati ya Imamu Hussein (a.s).
- - Kufungua vituo vya ziada kwa ajili ya kujibu maswali ya mazuwaru wanaokuja kufanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
- - Kurusha matangazo kwa njia ya video kwenye chanel ya Alkafeel na mtandao wa kimataifa Alkafeel, yenye maudui tofauti zinazo elezea tukio hili na malengo yake ya milele.
- - Kushiriki kwenye majlisi tofauti za kuomboleza ndani na nje ya Mkoa wa Karbala kupitia wahudumu wa kitengo.
- - Kuchapisha mafundisho mbalimbali na kuyagawa kwa mazuwaru, ndani ya ofisi za kitengo au kwenye maktaba zilizopo kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu.
- - Kushiriki kwenye harakati za kuomboleza zinazo fanywa na vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu.
- - Kuweka hadithi kwenye screen (tv) zilizopo ndani na nje ya haram zinazo husu ziara na malengo yake.
- - Kushiriki kwenye vipindi vya luninga na redio kwa kueleza malengo ya harakati ya bwana wa mashahidi (a.s).
- - Kujibu maswali yanayotufikia kwa njia za mitandao kupitia link: https://alkafeel.net/religious/index.php?add_quest au kwa simu namba: (009647706020688) au (009647803857576)".
Akamaliza kwa kusema “Tunaendelea na ratiba yetu mwezi wote wa Muharam, ratiba yetu inahatua tatu, kila hatua inasiku kumi hadi kuingia mwezi wa Safar”.