Kituo cha turathi za Basra kimekamilisha semina ya fani za uhakiki.

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, kimehitimisha semina ya fani za uhakiki wa nakala-kale na faharasi.

Semina ilikua na mihadhara saba yenye maudhui tofauti: (wakfu wa nakala za maandishi, mihuri, pembeni, utangulizi, uhakiki, nakala za maandishi, alama za nakala, ulinganishaji wa nakala za maandishi).

Semina imafanyika kuanzia tarehe (23/07/2022) hadi (31/07/2022) chini ya uhadhiri wa Ustadh Ahmadi Ali Majidi Alhilliy, semina imepata muitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi wa Dini na baadhi ya wadau wa turathi.

Tambua kuwa uongozi wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, umeshafanya semina nyingi kwenye sekta tofauti, kwa ajili ya kuongeza uwezo wa watumishi wake.

Tambua kuwa kituo cha turathi za Basra kipo mstari wa mbele katika kuhuisha aina zote za turathi za Basra na kuibua hazina zilizofichikana, kwani turathi hizo ni urithi wa kihistoria.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: