Shuhudia.. kitambaa kinacho ashiria huzuni za Ashura juu ya dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Katika kuonyesha huzuni na majonzi ya watu wa familia ya Mtume (a.s) katika mwezi huu, alio uawa mjukuu wa Mtume Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake, dirisha tukufu la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) limewekwa kitambaa kinacho ashiria majonzi ya Ashura.

Kitambaa hicho kinaumaalum wake tofauti na vitambaa vingine, kimechaguliwa kutoka katika vitambaa vya kifahari, sehemu ya kitambaa hicho imewekwa mawe ya vito (madini), kimezunguka dirisha pande zote nne, kama ifuatavyo:

  • - Upande wa mlango wa dirisha tukufu umeandikwa (Ewe mwenye kuhami watoto wa Fatuma), kwa juu yake kuna ufito wa (dhahabu) na kwenye paa kumeandikwa (Amani iwe juu yako ewe mlango wa haja).
  • - Upande wa Kibla umeandikwa (Amani iwe juu yako ewe mja mwema mtiifu kwa Mwenyezi Mungu, Mtume wake, kiongozi wa waumini na (Hassan na Hussein), juu yake kuna neno (Amani iwe juu yako ewe mnyweshaji wenye kiu Karbala).
  • - Upande mwingine umeandikwa (Amani iwe juu yako ewe mtoto wa muislamu wa kwanza, mtu wa kwanza kuamini mwenye msimamo zaidi wa Dini ya (Allah), yamefuatiwa na maneno yasemayo (Amani iwe juu yako ewe mnywesaji wenye kiu Karbala).
  • - Upande unaotazama mlango wa dirisha umeandikwa (Amani iwe juu yako ewe mwezi wa Bani Hashim), linafuatiwa na neno lisemalo (Amani iwe juu yako ewe mbeba bendera).

Maneno hayo yameandikwa kwa rangi ya njano na yamewekwa nakshi, kitambaa cha aina hiyo huwekwa kila mwaka unapoingia mwezi wa Muharam, kitengo kinachosimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya huchukua jukumu la kuweka kitambaa hicho.

Tambua kuwa kitambaa hakiwekwi kwenye dirisha pekeyake, bali tumebadilisha pazia zilizopo ndani ya haram tukufu, na kuweka pazia zinazo ashiria msiba zilizo wekwa nakshi na mapambo ya kifahari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: