Nitakulilia asubuhi na jioni.. Mawakibu za kuomboleza zinaendelea na maombolezo kwa siku ya tatu

Maoni katika picha
Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya toka asubuhi na mapema ya mwezi tatu Muharam, zimekua zikishuhudia mawakibu za kuomboleza zinazokuja kutoka kila upande wa mkoa mtukufu wa Karbala, zikiwemo maukibu za zanjeel, na maukibu za maatam huanza kuwasiri baada ya swala ya Magharibi na Isha.

Pamoja na kuongezeka kiwango cha joto, mamia ya waombolezaji wanashiriki kwenye maukibu hizo, wakiwa wamebeba bendera nyeusi na kupiga vifua vyao na kuonyesha huzuni kubwa kufuatia kifo cha mjukuu wa Mtume Imamu Hussein bun Ali (a.s), watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake, msiba ulioumiza Maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s).

Mawakibu hazijaishia kuomboleza pekeyake, bali kuna mawakibu za kutoa huduma kila sehemu, zimejipanga kwenye barabara zote zinazo elekea kwenye malalo takatifu.

Kumbuka kuwa mawakibu za kuomboleza zitaendelea kumiminika hadi siku ya mwezi kumi Muharam, kwa kufuata ratiba maalum iliyo andaliwa na kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: