Kufanya majlisi za kuomboleza kwa wanawake kwenye mitaa tofauti ya Karbala

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inafanya majlisi za kuomboleza kwa wanawake katika mitaa tofauti ya Karbala, kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hussein, watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake wema (r.a).

Kiongozi wa idara bibi Taghrida Tamimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa “Idara imeandaa ratiba ya kuomboleza msiba wa Imamu Hussein (a.s) na watoto wake watukufu, msiba ambao mbingu na ardhi zililia, wadudu na wanyama waishio majini walilia, na Malaika pia wakaweka vikao vya kuomboleza msiba huo mbinguni”.

Akaongeza kuwa: “Majlisi hizi zinafanywa chini ya maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, mwaka huu majlisi zimeongezeka na idadi ya wahadhiri pia imeongezeka, zinafanywa kwenye mitaa tofauti hususan ile iliyombali ambayo ni vigumu kwa wanawake kwenda kushiriki kwenye majlisi zinazo fanywa haram”.

Akafafanua kuwa: “Mitaa ya Karbala ambayo tunafanya majlisi za kuomboleza ni (eneo la Haafidh, Jariyya, Intifadha, mtaa wa Abbasi, eneo la njia ya Bagdad, karibu na jiko la Atabatu Abbasiyya, Towareji, Rashida, Albuwanani, Rajibiyya), majlisi hizi zinafanywa katika siku kumi za kwanza, tunamkakati mwingine wa kuendelea siku zingine zilizobaki katika mwezi”.

Akaendelea kusema: “Majlisi zinafanywa kwenye Husseiniyya na misikiti ya maeneo hayo, baada ya kuwasiliana na wenyeji, hufunguliwa kwa kusoma Qur’ani tukufu, ambayo hufuatiwa na mhadhara wa Dini unaoeleza harakati ya Imamu Hussein (a.s), kwa namna rahiri kueleweka sambamba na kuzingatia maelekezo ya Marjaa Dini mkuu, huhitimisha kwa kusoma kaswida za kuomboleza na dua faraji na kumpa pole Imamu wa zama (a.f).

Na utabaki # mwenendo wa Hussein
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: