Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu inafanya semina ya fani ya uhakiki

Maoni katika picha
Idara ya mambo ya hauza katika Maahadi ya Qur’ani tukufu mjini Najafu, chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya inafanya semina ya (Allama Albalaghi -r.a-) katika fani ya uhakiki wa nakala-kale.

Shekhe Kudama Hadharami kutoka idara ya tafiti za kihauza amesema “Zaidi ya wanafunzi ishirini wameshiriki kwenye semina ya siku sita, chini ya usimamizi wa Shekhe Karim Masira mkufunzi wa hauza, wamesoma misingi ya uhakiki, pamoja na kutambulisha vitabu vya zamani kwa lengo la kuongeza idadi ya wahakiki wa turathi za kiislamu”.

Akasema: “Maahadi ya Qur’ani tukufu inalenga kutambulisha turathi za kiislamu kwa ujumla, kwani kuna maelfu ya nakala-kale ambazo bado hazijajulikana wala kusomwa”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu inasimamia miradi mingi na semina za Qur’ani kwa wanafunzi na walimu wa vyuo vikuu na hauza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: