Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya kongamano la kujadili mkakati wa afya katika ziara ya Ashura

Maoni katika picha
Ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, umeshuhudia kongamano kubwa la kujadili maandalizi ya ziara ya Ashura ya Imamu Hussein (a.s) ambapo sekta ya afya ni sehemu muhimu ya maandalizi hayo.

Kongamano limehudhuriwa na mjembe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya sayyid Liith Najmu Mussawi na kiongozi wa idara ya afya, Pamoja na mkuu wa hospitali ya Alkafeel na mkuu wa idara ya Afya ya mkoa wa Karbala na Najafu bila kusahau wawakilishi wa idara ya usalama na mwezi mwekundu.

Katika kongamano hilo yamefanywa mapitio ya maandalizi na kuyaweka katika hatua ya utekelezaji, sambamba na kuandaa vitendea kazi, maandalizi haya yanatuwezesha kutoa huduma bora kwa raia na mazuwaru kabla na wakati wa ziara.

Tambua kuwa idara ya afya katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa mkakati kwa kushirikiana na idra ya afya ya mkoa wa Karbala, na kamati ya wataalam wa upasuaji, wizara ya afya, jumuiya ya mwezi mwekundu, wamejipanga kutoa huduma bora ya afya, sambamba na kuhakikisha usalama na amani kwa mazuwaru na kuwalinda wasipate maradhi ya kuambukiza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: