Siku ya Muharam saba hupewa jina la Abulfadhil Abbasi (a.s).. kwa nini?

Maoni katika picha
Wapenzi wa Ahlulbait (a.s) na wafuasi wao wanaohuisha siku za Ashura, wamezowea kuitenga siku ya saba katika mwezi wa Muharam, kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mtu anaweza kuuliza: kwa nini imekua hivyo?

Hakika kuchaguliwa siku ya saba kuwa maalum kwa ajili ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kunatokana na riwaya zinazosema kuwa, mwezi saba Muharam mwaka wa 61h, hali ilikuwa ngumu zaidi kwa familia ya Mtume (a.s) Abulfadhil Abbasi aliwaona watoto wa ndugu yake wanalia kiu.

Ndipo Abulfadhil Abbasi alipoamua kwenda kuchota maji kwa nguvu, akaondoka na wapanda farasi thelathini na watembea kwa miguu ishirini wakiwa na viriba ishirini, wakaelekea katika mto wa Furati wakitanguliwa na Naafii bun Hilali Almuradi, akasimama mbele yao kuwazuwia Amru bun Hajaaj Azubaidi, aliyekua kapewa jukumu la kulinda mto Furati, akawauliza: Mnafata nini hapa?

Akasema: Tumekuja kunywa maji mliyozuwia tusinywe.

Akamuambia: Kunywa.

Akamjibu: Ninywe wakati Hussein anakiu, pamoja na wafuasi wake?

Akasema: hauwezi kuwapelekea maji hao, hakika sisi tupo hapa kwa ajili ya kuzuwia wasipate maji.

Mashujaa katika wafuasi wa Imamu Hussein (a.s) hawakusikiliza maneno yake, wakaingia mtoni na kujaza viriba vyao maji, Amru bun Hajaaji na jeshi lake akataka kuwazuwia wasichote maji, ndipo jemedari wa Karbala Abulfadhil Abbasi (a.s) na Naafii Hilali, wakaingia vitani, wakapigana vita kali sana lakini hakuna aliyekufa pande zote mbili, wafuasi wa Imamu Hussein (a.s) chini ya uongozi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wakarudi wakiwa wamejaza maji vyombo vyao.

Abulfadhil Abbasi (a.s) akafanikiwa kuwapa maji wenye kiu siku hiyo, kuanzia siku hiyo akapewa jina la mnyweshaji (Saqaa) nalo ni miongoni mwa majina mashuhuri kwake, linajulikana zaidi kwa watu, pia ni jina pendwa sana kwake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: