Rais wa kitengo cha Maqaam hiyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Adnani Dhaifu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Watumishi wa kitengo chetu ni sawa na watumishi wengine wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), walianza kujiandaa kwa ajili ya tukio hili muda mrefu, chini ya utaratibu ulio wekwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya, kwa kuweka mazingira bora ya kufanya ibada na kuomboleza kwa watu wanaokuja katika eneo hili takatifu”.
Akaongeza kuwa: “Maandalizi yamefanywa kwa awamu bila kuathiri harakati za mazuwaru, tena kwa muda maalum, idara zote zimeshiriki kwenye maandalizi hayo, miongoni mwa maandilini ni:
- - Kusafisha sehemu zote za Maqaam na ukuta wa ndani na nje na maeneo Jirani.
- - Kutandika mazulia mapya.
- - Kukarabati mifumo yote ya Maqaam (viyoyozi – vipaza sauti – umeme – tahadhari) na mingineyo.
- - Kuweka alama zinazo ashuria huzuni ndani na nje ya Maqaam, ikiwa ni Pamoja na kufunika ukuta kwa vitambaa vyeusi, na kufunga vitambaa vyenye ujumbe wa kuomboleza vilivyo shonwa idara ya ushonaji chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri.
- - Kuwasha taa nyekundu zinazo ashiria huzuni.
- - Kuandaa kumbi kwa ajili ya kufanya majlisi za kuomboleza, upande wa wanaume na wanawake.
- - Kugawa maji ya kunywa na juisi za baridi kwa mazuwaru”.
Akaendelea kusema: “Pamoja na tuliyosema tumepokea watoa huduma wa kujitolea waliokuja kusaidia watumishi wa kitengo chetu kuwahudumia mazuwaru wanao endelea kuongezeka hadi siku ya mwezi kumi Muharam”.
Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vitengo vyake vyote, imeandaa utaratibu wa kupokea mazuwaru wa Ashura kuanzia siku ya kwanza hadi ya kumi, sambamba na kutoa huduma bora kwao.