Kama mkikataa tambueni mimi ni mtoto wa Hassan.. Usiku wa mwezi nane Muharam unashuhudia mambo yanayo umiza moyo

Maoni katika picha
Meli ya huzuni na majonzi imetia nanga katika ardhi ya Karbala leo mwezi saba Muharam na usiku wake, siku ambayo anakumbukwa Qassim mtoto wa Hassan (a.s), yanaangaziwa mapambano yake katika siku ya Ashura na kuuwawa kwake mbele ya Ammi yake Hussein (a.s).

Waombolezaji wamevaa nguo nyeupe na wamebeba mishumaa, jioni zimetoka mawakibu za Karbala ambazo hutoka jioni ya siku ya Ashura baada ya swala ya Ishaa wakiwa na watoto waliovaa nguo nyeupe, kijani na za rangi zingine, wengine wanakuja wamekaa juu ya farasi au wanatembea wakiwa wameshika farasi huku wanasema: (Kama mkikataa tambueni mimi ni mtoto wa Hassan mjukuu wa Mtume).

Kama ishara ya kujifananisha na Qassim (a.s) jinsi alivyo kwenda peponi, na watu wengine wamebeba vitu mbalimbali.

Matembezi hayo yamepita katika malalo ya Abulfadhil Abbasi na yakaishia kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s), huku wakiimba kaswida zinazotaja yaliyomtokea Qassim siku ya Ashura na kuuwawa kwake mbele ya Ammi yake Hussein (a.s), wakataja ushujaa wa kijana huyo na msimamo imara aliokua nao wa kumtetea Ammi yake Hussein (a.s).

Kumbuka kuwa siku ya mwezi nane Muharam sio siku aliyouwawa Qassim (a.s), yeye na watu wa nyumba ya Hussein (a.s) pamoja na wafuasi wake, waliuwawa mchana wa mwezi kumi Muharam, watu wa Karbala sawa na watu wengine duniani, kila siku huombolezwa mtu au watu maalum katika siku zote za uombolezaji, huo ndio utamaduni ambao wamerithi kizazi baada ya kizazi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: