Skauti ya Alkafeel imeandaa matembezi ya kuomboleza msiba wa Imamu Hussein (a.s) kwa wajumbe wake

Maoni katika picha
Jumuiya ya Skauti ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi katika kitengo cha Habari cha Atabatu Abbasiyya jana siku ya Jumamosi imefanya matembezi ya kuomboleza mauwaji yaliyofanyika Karbala ya Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake.

Kiongozi wa idara hiyo Sayyid Hasanaini Faariq ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa “Maandamano hayo ni sehemu ya maombolezo ya Imamu Hussein yaliyo anza siku chache zilizopita, yanalenga kufahamisha harakati ya Imamu Hussein (a.s) na kufanyia kazi mafundisho yake”.

Akaongeza kuwa: “Matembezi yalianzia katika eneo la mlango wa Bagdad, waombolezaji walisimama kwa mistari na kuanza kuimba kaswida za kuomboleza huku wakitembea hadi kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s)”.

Akaendelea kusema: “Baada ya hapo waombolezaji wakaelekea kwenye malalo ya mbeba bendera Abulfadhil Abbasi (a.s), walipo fika wakafanya majlisi ya kuomboleza ndani ya haram takatifu, wakasoma tenzi na mashairi yaliyo elezea ukubwa wa msiba huo”.

Kumbuka kuwa jumuiya ya Skauti ya Alkafeel hushiriki kwenye matukio mbalimbali ya uombolezaji na utoaji wa huduma, katika misimu ya uombolezaji na ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu, na hufanya program mbalimbali zinazolenga kutambulisha harakati na mafundisho ya Imamu Hussein (a.s) kwa wanachama wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: