Muhimu.. kupitia dirisha la ziara kwa niaba kwenye mtandao wa Alkafeel, inafanywa ziara maalum ya Ashura

Maoni katika picha
Idara ya Massayyid katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kuwa kesho siku ya Jumanne itafanya ziara ya Ashura maalum, kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) ya mwezi kumi Muharam, ziara hiyo ni kuhitimisha program ya idara ya teknolojia na taaluma za mitandao iliyoandaliwa na kitengo cha Habari kwa kushirikiana nao.

Watu watakaofanyiwa ziara ni wale waliojisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba katika mtandao wa kimataifa Alkafeel kwa link ifuatayo: https://alkafeel.net/zyara/ au kupitia App inayopatikana kwenye simu ganja za kisasa (smartphone): https://alkafeel.net/Apps/Arabic/.

Watafanyiwa ziara na kuswaliwa rakaa mbili na dua pamoja na ibada zingine, ibada hizo zitafanywa na Masayyid wanaotoa huduma katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kumbuka kuwa hii ni miongoni mwa program kubwa za kiibada na kiuombolezaji katika siku kumi za kwanza za mwezi mtukufu wa Muharam, inavipengele vingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: