Atabatu Abbasiyya tukufu imeongeza mita 1700 za mraba katika kuhudumia mazuwaru

Maoni katika picha
Kitengo cha ukarabati na ujenzi wa kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya, kimeandaa uwanja wenye ukubwa wa mita (1700) kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru, na kuongezwa kwenye uwanja uliokuwepo, kwa ajili ya kufanya ibada mbalimbali, hususan katika msimu wa ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu, ikiwemo ziara ya mwezi kumi Muharam.

Sehemu iliyo ongezwa kulikua na nyumba zilizo ondolewa pembeni ya ukuta wa Atabatu Abbasiyya, upande wa mlango wa Alqami na Imamu Ali (a.s), mlango wa mkono, mkabala na sehemu iliyopo kati ya mlango wa Furati upande wa kaskazini mashariki ya Ataba tukufu.

Tumefanya kazi ya kusawazisha ardhi na kuweka zege na marumaru.

Watumishi wa kitengo cha ukarabati na ujenzi wa kihandisi wamefanya kazi kubwa ya kuandaa sehemu hiyo, pamoja na ugumu wa hali ya hewa unaosababishwa na ongezeko la joto.

Kuna sehemu maalum imetengwa kwa ajili ya kutunza maji yanayogawiwa kwa mazuwaru siku ya ziara ya mwezi kumi Muharam, na sehemu nyingine ni maalum kwa ajili ya kufanya ibada mbalimbali.

Kumbuka kuwa mradi huu umefanywa kwa ajili ya kupunguza msongamano ambao hutokea sehemu hiyo, hasa wakati wa ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu, msongamano ambao hutatiza ufanyaji wa ibada zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: