Atabatu Abbasiyya yaandaa makumi ya mahodhi ya maji kwa ajili ya kuwapa mazuwaru na mawakibu

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa makumi ya mahodhi ya maji kwa ajili ya kugawa kwa mazuwaru, mawakibu za kuomboleza na washiriki wa matembezi ya Towajeri.

Hakika swala hili linatokana na maelekezo ya katibu mkuu wa Ataba tukufu Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini, amekiambiwa kiwanda cha maji cha Alkafeel kiandae kiwango hicho cha maji na kuyawaka sehemu muwafaka kwa ajili ya kugawa kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), yamewekwa kwenye moja ya viwanja vilivyo andaliwa hivi karibuni ili kuwa karibu na mazuwaru.

Sambamba na huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya kupitia idara ya maji, kwa kusambaza maji kwenye mawakibu na vituo vya Ataba, toka siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam na bado inaendelea, kila siku kazi inaongezeka kutokana na kukaribia kilele cha ziara na haja ya maji kutokana na kuongezeka kwa joto.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vitengo vyake vyote, imeandaa utaratibu maalum wa kutoa huduma na kupokea mazuwaru wa Ashura, kuanzia siku ya kwanza hadi ya kumi Muharam, kwa lengo la kutoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: