Wanafunzi wa Dini katika mji wa Karbala wanahuisha usiku wa kumi Muharam

Maoni katika picha
Wanafunzi wa Dini katika mkoa wa Karbala wamefanya matembezi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hussein (a.s) jioni ya leo siku ya Jumanne.

Kwenye matembezi hayo wameshiriki baadhi ya viongozi, walimu wa hauza, wanafunzi na kundi kubwa la watu waliojiunga wakati wa matembezi.

Matembezi yameanzia barabara ya Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakatembea hadi kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ambapo walisimama na kutaja yaliyotokea katika ardhi hiyo, kisha wakaelekea kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s), wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu, wakasisitiza kufuata mwenendo wake, huku wakiimba kaswida za huzuni na majonzi.

Kumbuka kuwa usiku wa kumi Muharam, ni tofauti na siku zingine, kuna mawakibu nyingi ambazo huja kuomboleza, miongoni mwa mawakibu hizo ni hii ya wanafunzi wa Dini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: