Vipi Hussein na watu wake waliutumia usiku wa Ashura

Maoni katika picha
Mwezi tisa Muhara, jeshi la maadui lilielekea kwenye hema za Imamu Hussein (a.s), Hussein alikua amekaa mbele ya hema lake…

Abbasi bun Ali akamuambia: Ewe ndugu yangu simama wamekuja.

Akasimama kisha akasema: Ewe Abbasi nenda kawaulize wanataka nini?

Abbasi akawafuata akiwa na wapanda farasi ishirini, akawauliza: Mnataka nini?

Wakasema: Imekuja amri kutoka kwa kiongozi, mnatakiwa kula kiapo cha utii au tuingie vitani.

Abbasi akarudi kwa Imamu Hussein (a.s), akamuambia kama walivyosema wale watu.

Hussein (a.s) akasema: Rudi ukawaombe watupe nafasi hadi kesho, watuachie usiku huu tuswali kwa ajili ya Mola wetu, tusome dua na kufanya istighfaar, hakika anajua mimi napenda kuswali na kusoma kitabu chake.

Abbasi akaenda na kuwaomba hilo, wakakataa.

Amru bun Hajaaj Zubaidi akasema: Ole wenu, naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu lau wangekua watu wengine tungewakubalia, kwa nini hawa tukatae wakati ni familia ya Muhammad?! (wakakubali).

Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake pamoja na watu wa nyumbani kwake wakakesha wanafanya ibada, huyu kasimama yule kakaa, mwingine karukuu, yule kasujudu, sauti zilisikika kama kundi la nyuki usiku kucha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: