Kuendelea kwa harakati za waombolezaji wa matembezi ya Towareji katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Harakati za waombolezaji wa matembezi ya Towareji zinaendelea katika Atabatu Abbasiyya tukufu, matembezi yanafanywa kwa utaratibu mzuri bila kutokea msongamano wowote.

Matembezi yanafanywa kama yalivyopangwa kupitia milango maalum kwa kuingia na kutoka, hakuna msongamano wowote unaotokea wakati wa uombolezaji huo, tumetumia mbinu ya kuweka watu maalum wanao simamia na kuongoza matembezi hayo.

Imetengwa milango mitatu maalum inayotumika kuingia washiriki wa maombolezo hayo, ambayo ni (mlango wa Imamu Hassan – Imamu Hussein – Imamu Mahadi), na milango ya kutokea ni (mlango wa Kibla – Amiir - Alqami – Imamu Haadi) inaelekea kwenye barabara zilizopo pembeni ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: