Kwa picha: Hivi ndio yalivyo kuwa matembezi ya kwanza ya waombolezaji wa Towareji

Maoni katika picha
Umekua utamaduni wa miaka mingi kuomboleza kwa kupitia matembezi ya Towareji, jambo hilo lilianzishwa na wakazi wa mji wa Towareji uliopo kilometa (20) kusini mashariki ya mkoa wa Karbala, waumini hukusanyika kwenye barabara inayoelekea Karbala karibu na eneo linalo itwa (Qantwara salaam).

Waombolezaji kutoka mji wa Towareji na Karbala na miji mingine ya Iraq hukusanyika hapo, idadi yao huwa zaidi ya milioni, hushiriki matembezi hayo watu kutoka nchi zingine pia, wote hupaza sauti za (Yaa Hussein.. yaa Hussein), sauti hiyo hupasua anga na kuonyesha mapenzi yao kwa Ahlulbait (a.s).

Kundi hilo huonyesha kama wanakuja kumnusuru Imamu Hussein (a.s), lakini wamechelewa na kukuta Imamu (a.s) kisha uwawa, hivyo hupiga vichwa vyao na kusema: (Yaa Hussein.. yaa Hussein).

Waombolezaji huanza matembezi yao katika eneo hilo la -Quntwara salaam- wakipitia barabara ya Jamhuriyya, hutembea kilometa kadhaa kabla ya kuwasiri kwenye malalo mbili takatifu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), matembezi hayo huishia katika malalo ya mnyweshaji wenye kiu Karbala (a.s).

Kamera ya mtandao wa Alkafeel inakuletea baadhi ya picha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: