Muhimu.. Atabatu Abbasiyya yatangaza kufanikiwa kwa mkakati wake wa ziara ya Ashura

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetoa tamko rasmi jioni ya Jumanne, kuhusu kufanikiwa kwa mkakati wake wa ulinzi na huduma katika ziara ya Ashura mwaka huu (1444h), ulioanza tangu Muharam mosi na ukaendelea hadi Muharam kumi, ifuatayo ni nakala ya tamko:

Amani iwe juu ya Hussein, na Ali bun Hussein, na watoto wa Hussein, na wafuasi wa Hussein, tunatoa salam za rambirambi kwa Imamu wa zama Hujjat bun Hassan (a.s) na Maraajii watukufu na ulimwengu wa kiislamu kwa ujumla, katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hussein (a.s), tunamuomba Mwenyezi Mungu ailinde miji ya waislamu na kila aina ya baya.

Kazi iliyofanywa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na wahudumu wa kujitolea waliokuja kutoka mikoa tofauti, imekuwa na mafanikio makubwa, watoa huduma wa kujitolea walikua zaidi ya (6000), maukibu zilizo shiriki ni zaidi ya (2200) huku jumla ya vyombo vya Habari vilivyo shiriki vikiwa (365), wote wamefanya kazi kwa utaratibu maalum.

Ziara ya mwaka huu imepangiliwa vizuri sana, kulikua na ushirikiano mkubwa kati ya mazuwaru na watumishi wa Ataba mbili tukufu, pamoja na wahudumu wa mawakibu Husseiniyya, wote kwa pamoja wametekeleza maagizo yaliyotolewa na Ataba mbili tukufu.

Pamoja na ongezeko la joto, tumefanikiwa kutoa huduma bora kulingana na uwezo tulionao, kila mtu amewajibika vivuri katika eneo lake na hakuna msongamano wowote uliotokea wakati wa ziara, lengo limefikiwa, nalo ni kuhakikisha mazuwaru wanafanya ziara kwa amani na utulivu, na baada ya ziara warudi salama majumbani kwao.

Kulikua na mawasiliano ya karibu sana kati ya wahudumu na vyombo vya ulinzi na usalama katika mji wa Karbala, ndio siri kubwa ya mafanikio haya, hakika ziara hii ni utangulizi wa ziara ya Arubaini.

Tunatoa shukrani za dhati kwa vikosi vya ulinzi na usalama, vikundi vya Husseiniyya, idara za kutoa huduma za kijamii hapa mkoani, watumishi wa Ataba takatifu, mawakibu Husseiniyya, idara za serikali na watoa huduma wa kujitolea, kwa kazi kubwa waliyofanya ambayo imesababisha kupatikana kwa mafanikio haya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: