Mjumbe wa ugeni huo na rais wa kitengo cha kusimamia haram ya Atabatu Abbasiyya bwana Khaliil Hanuun ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Atabatu Abbasiyya tukufu imetuma ugeni unao ongozwa na mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Afdhalu Shami akiwa na baadhi ya wahudumu wa malalo takatifu, walioenda kuchangia utoaji wa huduma katika eneo hilo takatifu”.
Akaongeza kuwa: “Mambo makuu tuliyofanya ni:
- - Kuandaa gari za kubeba mazuwaru kutoka mikoa tofauti na kuwapeleka Samaraa kwa ajili ya kufanya ziara hiyo kisha kuwarudisha baada ya ziara.
- - Tumegawa zaidi ya sahani elfu (10) za chakula kwa mazuwaru wa malalo takatifu kwa kushirikiana na mgahawa wa Atabatu Askariyya.
- - Kugawa zadidi ya mahodhi ya maji (4000) na mamia ya vipande vya barafu.
- - Kushiriki kwenye shughuli za uombolezaji ndani ya Atabatu Askariyya takatifu.
- - Kushiriki kwenye majlisi ya kuomboleza kwa kuhadithia kisa cha kuuwawa Imamu Hussein (a.s) ndani ya uwanja wa haram ya malalo ya Askariyaini (a.s).
- - Kuhuisha usiku wa kumi na moja Muharam (usiku wa msiba)”.
Akafafanua kuwa: “Ushiriki wetu wa mwaka huu umekua mkubwa, tumepeleka wajumbe wengi pia gari za Atabatu Abbasiyya tukufu zimepeleka watu wengi”.
Kumbuka kuwa jambo hili linafanywa kwa mwaka wa tatu mfululizo, hakika Atabatu Abbasiyya tukufu inaushiriki maalum kwenye matukio mengi na ziara tofauti zinazo fanywa kwenye haram hiyo takatifu ikiwemo ziara hii ya Ashura katika mwezi wa Muharam.