Kuanza kuandaa uwanja wa katikati ya haram mbili baada ya kukamilika ziara ya Ashura

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, jioni ya Jumanne, wameanza kazi ya kusafisha uwanja wa katikati ya haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na maeneo Jirani, baada ya kumaliza ibada ya ziara na matembezi ya towajeri ambayo huhudhuriwa na mamilioni ya watu.

Kazi hiyo wanashiriki watumishi wa kitengo na idadi kubwa ya wahudumu wa kujitolea, wanatandua zulia jekundu ambalo limetandikwa kwenye eneo la ukubwa wa mita za mraba elfu (14), sambamba na kuondoa vizuwizi vilivyo wekwa kwa ajili ya kuongoza matembezi ya maukibu ya Towareji.

Hali kadhalika kazi ya usafi umehusisha sehemu zilizo ezekwa pamoja na maeneo Jirani, sehemu hizo zitaendelea kutumika kwa matumizi mengine baada ya kukamilika ibada ya ziara.

Kumbuka kuwa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili kiliweka utaratibu maalum wa ulinzi na utoaji wa huduma katika ziara ya mwezi kumi Muharam, uliodumu kwa muda wa siku zote kumi, kulikua na mambo ya kufanywa wakati wa ziara, na baada ya ziara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: