Kwa vifua vilivyojaa huzuni.. Masayyid wanaotoa huduma wanampa pole shangazi yao jabali wa Subira

Maoni katika picha
Kwa huzuni na majonzi makubwa, Masayyid wanaotoa huduma katika Ataba takatifu za Karbala, wamefanya matembezi ya kuomboleza na kumpa pole shangazi yao jabali wa Subira bibi Zainabu (a.s), kwa kufiwa na ndugu zake na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Matembezi hayo yameanzia katika Maqaam ya hema la Imamu Hussein (a.s) wakiwa wamevua vitambaa vyao kama ishara ya kuonyesha ukubwa wa huzuni waliyo nayo kutokana na msiba huo unaoumiza umma wa kiislamu.

Watu waliokuwepo kwenye Maqaam ya hema la Imamu Hussein (a.s) pia wameshiriki kwenye matembezi hayo, zimesomwa tenzi na kaswida za huzuni kumpa pole bibi Zainabu (a.s) huku wakipiga vifua kwa huzuni ya kuuwawa kishahidi baba wa watu huru (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: