Kitengo cha uokozi Alkafeel kimetoa huduma kwa ustadi mkubwa katika ziara ya Ashura.
Kilisambaza watoa huduma ya afya waliokua tayali kutoa huduma za matibabu na kupeleka wagonjwa kwenye vituo vya afya na hospitali za karibu wakati wote.
Watoa huduma za uokozi na matibabu ya dharura wamewekwa kwenye makundi (38) yenye zamu mbili, asubuhi na jioni, wakiwa na gari za waginjwa pamoja na mawasiliano ya moja kwa moja na vituo vya afya.
Vikosi vimewekwa kwenye maeneo tofauti: ndani ya jengo tukufu la haram na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili.
Tambua kuwa watoa huduma hao wamepata mafunzo ya nadharia na vitendo.
Kumbuka kuwa idara ya uokozi na huduma ya kwanza ikochini ya kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu.