Watumishi wa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili wamemaliza kazi ya kusafisha uwanja huo

Maoni katika picha
Watumishi wanaosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili chini ya Atabatu Abbasiyya, wamemaliza kazi ya kusafisha uwanja huo, baada ya ziara ya Ashura.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naafii Mussawi amesema: “Wahudumu wetu walianza kazi ya kusafisha uwanja wa katikati ya haram mbili asubihi ya Jumatano mwezi kumi na moja Muharam”. Akaongeza kuwa “Wamefanya kazi kwa bidii na wamemaliza ndani ya muda mfupi”.

Akaendelea kusema: “Tumetandua mazulia yaliyokua yametandikwa kwenye eneo lenye ukubwa wa mita za mraba (14000) pamoja na nailoni iliyokua chini yake” akasema: “Kisha tukapiga deki kwa kutumia vifaa maalum”.

Kumbuka kuwa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili chini ya Ataba mbili tukufu, ni sawa na vitengo vingine vya Ataba, kimefanya kazi kubwa ya kuhudumia mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara ya Ashura.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: