Watu 161,699 wamefanyiwa ziara ya Ashura kwa niaba kupitia mtandao wa Alkafeel

Maoni katika picha
Idadi ya watu waliojisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba katika mtandao wa kimataifa Alkafeel na App zake imefika (161,699) kutoka ndani na nje ya Iraq, wamefanyiwa ziara ya Ashura kwa niaba.

Kiongozi wa idara ya teknolojia na taaluma za mitandao chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Haidari Twalibu Abdul-Amiir amesema: “Ziara ya Ashura mwaka huu kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba imekua na muitikio mkubwa tofauti na miaka ya nyuma, hufanywa kwa kushirikiana na idara ya Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Asilimia kubwa ya watu waliojisajili wanatoka katika nchi zifuatazo: (Iraq, Sudani, Falme za kiarabu, Yemen, Qatar, Moroko, Misri, Ajeria, Baharain, Saudia, Kuwait, Oman, Tunisia, Iran, Lebanon, Pakistan, Urusi, Marekani, Uingereza, India, Swiden, Kanada, Malezia, Australia, Ujurumani, Islandi, Namsa, Yunani, Holandi, Denmak, Norwey, Ubelgiji, Afughanistani, Ekwado, Brazili, Ajentina, Uswisi, Naijeria, Gana, Indonesia, Italia, Hispania, Ufaransa, Uturuki, Adharbaijani, Qabrusi, Finlendi, China, Ealendi, Honkon na Japani)”.

Akafafanua kuwa: “Kazi hiyo ilihitimishwa mwezi kumi Muharam kwa kufanya ziara maalum ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na swala ya rakaa mbili na dua, usajili ulifanywa kupitia lugha zote zulizopo kwenye mtandao wa kimataifa Alkafeel, ambazo ni: (Kiarabu, Kiengereza, Kiurdu, Kituruki, Kifaransa, Kifarsi, Kiswahili na Kijerumani)”.

Kumbuka kuwa hii ni miongoni mwa ratiba kubwa ya kiibada na kiuombolezaji katika siku kumi za kwanza za mwezi mtukufu wa Muharam, na inavipengele vingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: