Kituo cha Dirasaati Afriqiyyah kimefanya matembezi ya wapenzi wa Hussein

Maoni katika picha
Kituo cha Dirasaati Afriqiyyah chini ya kitengo cha Habari na utabaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya matembezi ya wafuasi wa Husseini Alasiri ya jana siku ya Alkhamisi mwezi (12 Muharam 1444h) sawa na tarehe (11 Agosti 2022m) kwa waafrika waliopo Iraq, wameshiriki wanafunzi wa kiafrika wanaokaa Najafu na Karbala.

Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataaru Shimri ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa “Kutokana na umuhimu wa kuhuisha maadhimisho ya Husseiniyya na kumpa pole kiongozi wa waumini (a.s) na mjukuu wake Imamu wa zama, tumefanya matembezi haya ya (wapenzi wa Hussein) wenye asili ya Afrika wanaoishi Iraq”.

Akaongeza kuwa: “Matembezi yalianzia katika eneo la uwanja wa Maidani hadi kwenye malalo ya kiongozi wa waumini (a.s), sehemu ambayo waombolezaji wametao pole za msiba huu na kupandisha bendera za mataifa yao na kula kuiapo cha utii”.

Akabainisha kuwa: “Washiriki wamepongeza matembezi haya kuandaliwa na Markazi dirasaati Afriqiyyah, wakasema imekua mstari wa mbele kusaidia familia za waafrika hapa Iraq, huandaa majlisi za kuomboleza na kuwasiliana nao wakati wote, sambamba na kufanya miradi ya kibinaadamu na kidini katika bara la Afrika.

Kumbuka kuwa ratiba hii ya Ashura itafanywa kila mwaka, kama sehemu ya ratiba ya Markazi katika maadhimisho ya Husseiniyya kwenye bara la Afrika na hapa Iraq, kutakua na harakati maalum kuhusu maombolezo ya Imamu Hussein (a.s) katika kipindi cha miezi miwili ya uombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: