Baada ya kumaliza shughuli za ziara ya Ashura.. zinatolewa alama zilizowekwa kwenye milango ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Asubuhi ya Jumamosi, watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wameanza kazi ya kutoa alama zilizowekwa kwa muda kwenye milango ya Ataba wakati wa ziara ya Ashura kwa ajili ya kuongoza matembezi ya mawakibu na mazuwaru.

Kazi hiyo imefanywa sambamba na kutandua mazulia yaliyo wekwa kwa muda kwenye milango saba, mitatu upande unaotazamana na uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu iliyotumika kuingilia mawakibu ambayo ni (Mlango wa Imamu Hassan – Imamu Hussein na Imamu Mahadi) na minne ilyotumika kutokea ambayo ni (Mlango wa Kibla – Amiir – Alqami na Imamu Haadi).

Tambua kuwa milango hiyo iliandaliwa maalum kwa ajili ya kurahisisha uingiaji na utokaji wa mawakibu, na kuhakikisha hakuna msongamano wowote unaotatiza harakazi za mazuwaru sambamba na kuwezesha kuingia na kutoka kwa urahisi mamilioni ya waombolezaji.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu iliweka utaratibu maalum wa utoaji wa huduma kwa mazuwaru wa Ashura, ulianza kutumika tangu siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Muharam na ukaendelea hadi mwezi kumi na tatu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: