Kazi ya kusafisha Atabatu Abbasiyya na sardabu zake imeanza

Maoni katika picha
Wahudumu wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wameanza kazi ya kusafisha uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na njia zinazo elekea kwenye haram pamoja na sardabu zake, baada ya kumaliza shughuli za ziara ya Ashura.

Usafi umefanywa kwa awamu katika maeneo yeto ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), tumeanza kutandua mazulia kisha tukapiga deki na kutandika mazulia mapya, sambamba na kuondoa vizuwizi vilivyo wekwa kwa ajili ya kuongoza matembezi ya mazuwaru.

Tumesafisha pia barabara zote zinazo elekea Atabatu Abbasiyya na viwanja vinavyo zunguka Ataba takatifu, sambamba na maeneo ya bustani na vituo vya maji, tumetumia vifaa vya kisasa na watumishi wenye ufanisi katika kazi yao.

Kumbuka kuwa usafi ni kazi ambayo hufanywa na kitengo hiki kila siku, mara tu baada ya kumaliza shughuli za ziara ya Ashura kazi ya kusafisha maeneo yote ikaanza mara moja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: