Haram takatifu ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) jioni ya jana siku ya Jumamosi, imeshuhudia kazi kubwa ya usafi na kutandikwa mazulia mapya, baada ya kumaliza shughuli za maombolezo zilizodumu kwa muda wa siku kumi na tatu, katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustwafa Murtadha Aali-Dhiyaau-Dini na baadhi ya viongozi wameshiriki kwenye kazi ya kufanya usafi huo.
Kiongozi wa Idara ya haram bwana Nizaar Ghani Khaliil amesema: “Kazi za ndani ya haram tukufu zimehusisha kusafisha na kutandika mazulia kuanzia kwenye dirisha tukufu, tunatumia vifaa maalum, baada ya kusafisha dirisha tukaelekea kwenye korido nne zinazo zunguka dirisha”.
Akaongeza kuwa “Tumesafisha sakafu, kuta, na kuondoa vitu vilivyo wekwa kwa ajili ya ziara ya Ashura, kisha tukatandika mazulia maalum yaliyo andaliwa kwa ajili ya eneo hilo”.
Naye makamo rais wa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu Zainul-Aabidina Adnani Quraishi amesema “Kazi hizo zimefanywa baada ya kutandua mazulia maalum yaliyotandikwa wakati wa ziara ya Ashura na kwenda kuyaosha, kuanzia yale yaliyokua nje ya haram tukufu hadi yale yaliyotandikwa kwenye milango ya Ataba tukufu”.
Akaongeza kuwa: “Baada ya kutandikwa ukumbi wa haram, mazulia mapya yamerudishwa, na mapambo yake ya kawaida yaliyo andikwa ziara na dua, mazingira yamerudi katika hali ya kawaida kama yalivyokua kabla ya ziara”, akaashiria kuwa “Wameshiriki watumishi wa idara ya kusimamia haram na kitengo chetu pamoja na wahudumu wa kitengo cha utumishi na masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Kumbuka kuwa kazi hii hufanywa kila mwaka baada ya kumaliza ziara ya Ashura, kazi hufanywa usiku wa manane, kwani muda huo idadi ya mazuwaru huwa ndogo jambo ambalo hurahisisha kazi ya usafi.