Kuendelea kwa ratiba ya warsha kwa walimu wa Al-Ameed

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kinaendelea kutoa semina na warsha za kuwajengea uwezo walimu wa shule za Al-Amiid.

Program hiyo inalenga kujenga uwezo wa walimu na kuboresha vipaji vyao, kwa kutumia mbinu za kisasa katika ufundishaji.

Kwa kiwango kikubwa semina inahusu utumiaji wa nyenzo katika kuwasilisha mada na kuifanya ieleweke, sambamba na kuongeza weledi wa walimu kwenye nyanja zote.

Program hiyo ni sehemu ya harakati ya kitengo cha malezi na elimu.

Kumbuka kuwa kitengo cha malezi na elimu ya juu hufanya semina, warsha na mashindano ya kielimu kwa lengo la kujenga uwezo wa watumishi wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: