Sahani za chakula 448,698 zimetolewa na mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye ziara ya Ashura

Maoni katika picha
Kitengo cha mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kuwa sawahani za chakula walizogawa kwenye ziara ya Ashura zilifika (448,698), kuanzia mwezi mosi hadi kumi na tatu, sambamba na aina zingine za vyakula, kila siku milo mitatu.

Rais wa kitengo hicho Mhandisi Aadil Hamaami ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mkakati wetu wa kugawa chakula kwa mazuwaru wa Ashura umedumu kwa muda wote wa ziara, idadi iliongezeka mwezi kumi hadi kumi na tatu Muharam siku ya maombolezo ya bani Asadi, hufanya hivyo kwenye kila msimu wa ziara, lakini msimu huu umeshuhudia idadi kubwa ya mazuwaru iliyopelekea kuongeza huduma ya chakula”.

Akaongeza kuwa: “Pamoja na milo mitatu ya chakula inayotolewa kila siku, tumetoa maji zaidi ya lita laki nne na elfu ishirini, matunda tani (7000) vitafunwa (halwa) pisi (9370), kazi ya kugawa imefanywa mfululizo kila siku”.

Akafafanua kuwa: “Ugawaji umefanywa kupitia sehemu mbili muhimu: sehemu ya kwanza ni kwenye lango la Bagdad kuelekea katika mji wa Karbala, na sehemu ya pili ni lango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), sehemu hizo hushuhudia msongamano mkubwa wa mazuwaru na mawakibu”.

Akabainisha kuwa “Ugawaji wa chakula umefanywa kwa kutumia vifungashio vya kutumika mara moja (take away), watu walisimama mistari miwili, mstari wa wanaume na wanawake, chakula kilichotolewa kinaendana na mahitaji ya watu kwa milo yote mitatu”.

Kumbuka kuwa ugawaji wa chakula kwa mazuwaru ni sehemu ya utaratibu wa Atabatu Abbasiyya wakati wa msimu wa ziara maalum ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kazi huyo hufanywa na vitengo vya kutoa huduma, na kitengo cha mgahawa huwajibika kuandaa chakula kila siku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: