Namna gani alivyokemea bibi Zainabu (a.s) Ibun Ziyaadi na wapambe wake katika siku kama ya leo mwaka wa 61h

Maoni katika picha
Wanahistoria wanasema sema kuwa, jeshi la ibun Ziyaadi liliporudi na kuingia kwenye jengo la utawala, waliweka mbele yake kichwa kitakatifu cha Imamu Hussein (a.s), akawa anachoma choma meno ya Imamu Hussein (a.s) na fimbo aliyokua nayo mkononi.

Zaidu bun Arqamu akamuambia: Ondoa fimbo yako kwenye midomo hiyo mitakatifu, naapa kwa haki ya Allah nilimuona Mtume (s.a.w.w) anabusu midomo hiyo, kisha akalia. Ibun Ziadi akamuambia: Mwenyezi Mungu ayalize macho yako, Wallahi kama usingekua mzee uliyepoteza akili ningekata shingo lako.

Zaidu akatoka huku anasema: Mtu kachukua utawala wa kurithi, enyi waarabu mmekua watumwa baada ya leo, Mmemuua mtoto wa Fatuma na kumtawalisha mtoto wa Marjanan, mmeua mbora wenu na kumtawalisho muovu wenu, mmeridhia udhalili, awe mbali anaeridhia udhalili.

Ibun Ziyadi alipoona watu wanaanza kubadilika, hasa alipozungumza na bibi Zainabu, aliogopa hasira za watu, akawaambia askari wawapeleke mateka kwenye nyumba ndogo pembeni ya msikiti, akasema ibun Ziyaadi: Nilikua pamoja nanyi ilipoamriwa muingizwe jela, nikaona watu wanaume kwa wanawake wamekusanyika wanalia na kupiga nyuso zao.

Zainabu akaongea kwa sauti ya juu mbele ya watu: Asiingie kwetu ispokua mtumwa au Ummul-Walad, hakika wao ni mateka kama sisi.

Aliashiria kuwa mateka anajua tabu za kutekwa, hakuna anayejua udhalili wa kutekwa ispokua mateka, na huo ndio ukweli usiopingika.

Ibun Ziyaadi akawaita kwa mara nyingine, walipoingia kwake, wakaona kichwa cha Imamu Hussein (a.s) kipo mbele yake, kinatoa nuru hadi mbinguni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: