Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hussein (a.s).
Mkuu wa Maahadi Shekhe Jawadi Nasrawi amesema: “Hii ni moja ya majlisi ambazo hufanywa kila mwaka, Maahadi imezowea kuifanya katika siku kama hizi, ambazo ulishuhudiwa msiba mkubwa katika historia ya umma wa kiislamu”.
Akaongeza kuwa: “Majlisi zitadumu kwa muda wa siku tano, zinahudhuriwa na wanafunzi wa mradi wa Qur’ani pamoja na watumishi wa Maahadi”. Akafafanua kuwa: “Siku ya kwanza mhadhiri alikua ni Shekhe Ali Muhani kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, aliongea kuhusu shuhuda za aya za Qur’ani alizotumia Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake”.
Akaendelea kusema: “Majlisi imeshuhudia usomwaji wa tenzi na kaswida zinazo muhusu Imamu Hussein (a.s) katika siku ya kwanza, na litaendelea kushuhudiwa hilo katika siku zingine zilizo baki”.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu kupitia ratiba hii, inatengeneza mazingira mazuri kwa wanafunzi na kuwajulisha kuwa Qur’ani na kizazi cha Mtume (s.a.w.w) ni vitu viwili visivyo tofautiana.