Watumishi wa Ataba mbili tukufu wanaadhimisha siku ya saba toka kuuwawa kishahidi kwa Imamu Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Siku ya Jumanne mwezi (17 Muharam 1444h) sawa na tarehe (16/08/2022m), yamefanywa matembezi ya kuomboleza kutoka haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi Atabatu Husseiniyya, maukibu maalum ya watumishi wa Ataba mbili tukufu kwa ajili ya kuomboleza siku ya saba tangu alipouawa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake watukufu.

Wamefanya matembezi hayo wakiwa wamebeba bendera nyeusi zilizo andikwa maneno ya kuomboleza, matembezi yameanzia ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakapita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, wakaenda hadi kwenye haram ya Imamu Hussein, wakaingia kupitia mlango wa Shuhadaa huku wanaimba kaswida na kuomboleza msiba huo.

Maukibu hiyo imetanguliwa na Masayyid pamoja na baadhi ya mashekhe watukufu wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya, matembezi hayo yakaishia ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein kwa kufanya majlisi ya kuomboleza.

Kumbuka kuwa Ataba tukufu za Karbala hufanya matembezi maalum ya kuomboleza kwenye kila tukio la msiba wa Ahlulbait (a.s) mwaka mzima, ambayo huanzia ima ndani ya Atabatu Husseiniyya kwenda Atabatu Abbasiyya na kinyume chake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: