Watu wa Karbala wanaomboleza siku ya saba tangu kuuwawa kishahidi Imamu Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Watu wa Karbala tukufu siku ya Jumanne mwezi (17 Muharam 1444h) wamefanya maukibu kubwa kuomboleza kifo cha Imamu Hussein (a.s), huo ndio utamaduni wa watu wa mji huu katika kuomboleza siku hiyo kila mwaka.

Rais wa kitengo cha Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Sayyid Aqiil Yasiriy amesema: “Watu wa Karbala wanafanya uombolezaji waliorithi kwa baba na babu zao, vimeshiriki vikundi tofauti vya waombolezaji, katika kuhuisha siku ya saba tangu alipouwawa Imamu Hussein, watu wa numbani kwake (a.s), na wafuasi wake”.

Akaongeza kuwa: “Maombolezo ya watu wa Karbala ya leo ni utamaduni wa kila mwaka wa wakazi wa mji huu, wamerithi vizazi na vizazi, aina hii ya kuomboleza msiba wa Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Wameanza kufanya matembezi baada ya swala ya Ishaa kwenye barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s), hadi kwenye haram ya Imamu Hussein, wakiwa wamebeba mishumaa na kuimba kaswida za kuomboleza, kisha wakaelekea katika Atabatu Abbasiyya wakipita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu.

Matembezi hayo yakaishia kwenye ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kufanya majlisi ya kuomboleza iliyohutubiwa na Mheshimiwa Shekhe Bahaau Karbalai, baada yake zikasomwa kaswida na tenzi mbalimbali kutoka kwa wahadhiri na washairi ambao wametoa mchango mkubwa katika kuhuisha tukio hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: