Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Bagdad chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imeanza utekelezaji wa mradi wa kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu.
Mradi huu unasimamiwa na walimu mahiri katika sekta ya kuhifadhi, semina inafanywa siku mbili za kuhudhuria moja kwa moja darasani kwa wiki na siku zingine wanafundishwa kwa njia ya mtandao.
Mradi huu umeanza sambamba na msimu wa msiba wa Husseini.
Tambua kuwa tawi la Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Bagdad, hufanya harakati mbalimbali zinazohusu Qur’ani pamoja na semina za mara kwa mara hapa mkoani.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani kupitia matawi yake tofauti ni sehemu ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, yenye jukumu la kufundisha Qur’ani takatifu.