Toleo la ishirini na mbili la jarida la (Alkhat-wah)

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha turathi za Basra, chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kimetoa jarida la ishirini na mbili (22) la (Alkhat-wah).

Toleo hilo limeandika maudhui mbalimbali zinazo husu turathi za mji wa Basra, viongozi wake na matukio yake.

Waandishi tofauti waliobobea kwenye mambo ya turathi, wameandika makala zao kwenye toleo hilo.

Tambua kuwa jarida la Alkhat-wah limefungua milango kwa kila mtu anayeandika kuhusu turathi za Basra, wasimamizi wake wanaamini umuhimu wa kuwa na mada tofauti.

Kumbuka kuwa jarida la (Alkhat-wah), ni jarida la kitamaduni linalo tegemea weledi wa waandishi wa kiiraq, limekua likitolewa na kituo cha turathi za Basra kwa miaka mingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: