Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imehitimisha semina ya Qur’ani katika mji wa Kaduna nchini Naijeria.
Mkuu wa kituo Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema: “Semina imefanywa kwa muda wa siku thelathini, wamefundishwa usomaji sahihi wa Qur’ani, Aqida, Fiqhi na Sira, washiriki walikua ni wanafunzi (100) wa jinsia zote, semina hiyo imesimamiwa na wawakilishi wa Markazi katika mji wa Kaduna, ambao ni Shekhe Shamsudini na Shekhe Ibrahimu Mussa”.
Akaongeza kuwa: “Semina inalenga kujenga uwelewa wa Dini na Aqida kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) na wapenzi wao katika jamii ya waafrika na kubainisha utukufu wa Ahlulbait (a.s) kwa njia rahisi inayo endana na uwezo wa walengwa”.
Akasisitiza kuwa: “Markazi inaendelea kufanya semina mbalimbali za mambo ya Dini, Aqida na Qur’ani tukufu katika bara la Afrika kwa wanafunzi wenye umri tofauti”.
Akamaliza kwa kusema: “Semina hiyo ndio mwanzo wa kufanywa semina zingine, imeshuhudia muitikio mkubwa kutoka kwa washiriki, jambo hilo litatufanya tujumuishe washiriki wenye umri tofauti, kwa lengo la kutumikia kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi kitakatifu (a.s)”.
Kumbuka kuwa Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya harakati mbalimbali katika bara la Afrika, zikiwemo semina hizi ambazo zinaimarisha mawasiliano na nchi za Afrika, sambamba na kutengeneza kizazi chenye maarifa ya Qur’ani tukufu na Ahlulbait (a.s).