Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu inaendelea na semina za kujenga uwezo wa walimu

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inaendesha semina ya kujenga uwezo wa walimu, ambayo jumla ya walimu hamsini wameshiriki.

Mkuu wa Maahadi Sayyid Muhandi Almayali amesema: “Wamefundishwa kusimama na kuanza, mbinu za ufundishaji, mbinu za kuhifadhisha, maswala ya Imla, sauti na naghmah, visa vya Qur’ani, wakufunzi ni walimu waliobobea kutoka hauza na kwenye vyuo vikuu vya Iraq, wamesoma kwa muda wa siku saba, kila siku ilikua na mihadhara mitatu”.

Akaongeza kuwa: “Kwenye semina hii wameshiriki zaidi ya walimu hamsini, na tunatarajia ndio mwanzo wa kufanya semina zingine kama hii, ili kupanua wigo wa usomaji wa Qur’ani katika jamii”. Akabainisha kuwa “Kuboresha uwezo wa mwalimu kutaleta matokeo mazuri kwa wanafunzi na kusaidia kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii”.

Akaendelea kusema: “Washiriki wa semina hii watafanya mitihani miwili, mmoja ni kwa vitendo na mwingine wa nadhariyya, kisha watapangwa kutokana na viwango vyao kwenye semina zingine za kuwajengea uwezo, tutaendelea kuwanoa hadi wawe walimu bora watakao endesha semina kama hii kwenye wilaya na mitaa”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu hufanya semina za Qur’ani kipindi chote cha mwaka, kupitia semina hizo imetoa mamia ya wahitimu miongoni mwa walimu na wanafunzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: