Kituo cha Alfadhil cha kulinda na kuhifadhi turathi kinafanya semina kwa watumishi wa kamati ya mambo na uadilifu

Maoni katika picha
Kituo cha Fadhil cha kulinda na kuhifadhi turathi za maandishi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya semina kwa watumishi wa kamati ya mambo na uadilifu kwa lengo la kuhifadhi nakala-kale zinazo milikiwa na kamati hiyo.

Msaidizi wa kiongozi wa kituo hicho Sayyid Ali Muhammad Jaasim amesema: “Semina imedumu kwa muda wa siku tano, wamefundishwa namna ya kukarabati na kutunza nakala-kale mbalimbali walizonazo”.

Sayyid Jaasim Tamimi kutoka kamati ya mambo na uadilifu amebainisha kuwa “Kamati inavielelezo zaidi ya laki saba na elfu hamsini (750,000) vinavyo hitaji kukarabatiwa na kutunzwa, kwa kusaidiana na Atabatu Abbasiyya tukufu tumefanikiwa kuwapa semina watumishi wa kituo cha Alfadhil, itakayo wawezesha kuhifadhi na kutunza turathi hizo kwa weledi”.

Kumbuka kuwa kituo cha Alfadhil cha kukarabati na kutunza turathi za nakala-kale, ni moja ya vituo vilivyo chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: