Chuo kikuu Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimepata nafasi ya (6957) duniani kwa mujibu wa taasisi ya (Webometrics) inayo husika na kupima viwango kimataifa.
Huku kikiwa chuo cha (62) katika vyuo vya Iraq na chuo cha (1745) duniani, wakati mwanzoni mwa mwaka huu kilikua chuo cha (8702) kimataifa.
Ulinganishaji uliofanywa hivi sasa ni wa nusu mwaka, hutumia mitandao yake katika ulinganishaji huo.
Kumbuka kuwa taasisi ya (Webometrics) ndio taasisi kubwa duniani inayopima ubora wa vyuo vikuu, inazaidi ya vyuo vikuu (20,000) duniani, hutoa taarifa yake kila baada ya miezi sita (mwezi wa Februari na Agosti), lengo kuu ni kuboresha viwango vya elimu kwenye vyuo vikuu na kuhimiza usambazaji wa majarida ya kielimu.
Tambua kuwa maendeleo yaliyopatikana yanatokana na juhudi za wanachuo na uandishi wa tafiti za kielimu kwenye majarida ya kimataifa, na kuboresha nyenzo za utoaji wa tafiti kwa njia za mitandao.