Majmaa Afaaf ya wanawake.. inatoa huduma tofauti za kujibu mahitaji wa mwanamke

Maoni katika picha
Majmaa Afaaf ya wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ni moja ya miradi mukubwa inayojibu mahitaji wa mwanamke, hufanya semina mbalimbali za ujasiliamali kwa wanawake na kuwaingiza soko la ajira.

Kiongozi wa Majmaa hiyo bibi Asmaa Al-Abadi amesema: “Wadau wa Majmaa hii wanatambua kuwa tumejikita katika kutoa huduma kwa wanawake tu, tunasaidia mwanamke wa kiiraq kijamii, kifamilia na kiajira”, akaongeza kuwa “Majmaa inavitengo vingi na bidhaa tofauti zenye ubora mkubwa sawa na zile zinazopatikana kwenye masoko makubwa duniani, na zinauzwa kwa bei nafuu”.

Akafafanua kuwa: “Majmaa haiishii kwenye kujibu mahitaji ya wanawake tu, bali hufanya mambo mbalimbali ya kusaidia jamii, kama vile kutoa semina za ujasiliamali na huduma kwa wateja, mafunzo ya ushonaji, mambo ambayo humuwezesha msichana kuingia kwenye soko la ajira moja kwa moja”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: