Rais wa Majmaa ya Qur’ani tukufu amesema: Tunajali ulinzi wa jamii kifikra

Maoni katika picha
Rais wa Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Mushtaqu Ali amesema kuwa Ataba tukufu inajali swala la kulinda jamii kifikra kupitia taasisi za Qur’ani na taasisi za kitamaduni.

Katika ujumbe aliotoa kwa washiriki wa semina ya kujenga uwezo iliyofanywa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu, amesisitiza kuwa “Semina hii ni muhimu kwa sababu imelenga walimu wa malezi ya kiislamu katika jamii ya wasomi wa sekula”.

Akasema “Elimu ya kiislamu inayotolewa kwenye semina hii inatakiwa iakisi mwenendo wa mwanafunzi katika kauli na vitendo vyao, na kujenga jamii yenye maarifa ya misingi ya Dini tukufu ya kiislamu”.

Akaendelea kusema: “Changamoto iliyopo kwenye jamii zetu ni vita ya kifikra na kitamaduni, kupitia vyombo vya Habari, yatupasa sisi sote kupambana na changamoto hiyo, kwa kufundisha itikati sahihi kwa vijana wetu, hususan kwa wanafunzi kwani wao ndio mustakbali wa umma”.

Akasisitiza kuwa “Semina za kielimu na makongamano ya kitamaduni pamoja na harakati zingine zinazo saidia kujenga fikra na utamaduni ni muhimu sana”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: