Kiongozi mkuu wa kisheria atoa zawadi kwa jopo la Majmaa ya Qur’ani

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amewapa zawadi watumishi wa Majmaa ya Qur’ani.

Watumishi hao walikua pamoja na rais wa Majmaa ya Qur’ani Dokta Mushtaqu Ali, waliopewa zawadi ni viongozi wa kituo cha miradi ya Qur’ani ambao ni: Hasanaini Halo, kiongozi mtendaji wa mradi wa kiongozi wa wasomaji, msomaji Muhammad Ridhwa Azubaidi, Faisal Matwaru, Waaidu Tamaari Maitham aliyeshunda kwenye shindano la kitaifa la wanafunzi wa sekondari, upande wa kuhifadhi Qur’ani tukufu, shindano ambalo ni sehemu ya kujiandaa na shindano la kimataifa.

Kikao hicho kimehudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa na mjumbe wa kamati kuu bwana Jawadi Hasanawi na kiongozi wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria dokta Afdhalu Shami.

Zawadi hii ni sehemu ya kuwatia moyo washiriki wa miradi ya inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, hususan miradi ya Qur’ani.

Kumbuka kuwa Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya inafanya miradi mingi inayohusu Qur’ani kwa lengo la kuandaa kizazi chenye uwelewa wa Qur’ani tukufu na uwezo wa kuifanyia kazi kwa kauli na vitendo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: