Jumuiya ya Skaut Alkafeel imeandaa hema la Skaut kwa watumishi wa Atabatu Askariyya

Maoni katika picha
Jumuiya ya Skaut Alkafeel chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya, imeandaa hema la Skaut kwa ajili ya watumishi wa Atabatu Askariyya tukufu.

Kiongozi wa kitengo cha Habari na mahusiano bwana Yunusi Ashuur amesema: “Lengo la ratiba hii ni kuwajengea uwezo washiriki” akaongeza kuwa “Kutakua na mashindano ya kielimu na kitamaduni, ratiba hiyo itadumu kwa muda wa siku tatu”.

Naye makamo kiongozi wa mambo ya kijamii katika Atabatu Abbasiyya, bwana Izudini Mustwafa amesema kuwa “Kushirikiana na jumuiya ya Skauti Alkafeel kunatokana na ubora wa Skauti hiyo”.

Akaendelea kusema “Lengo la kuja kwao ni kujenga uwezo wa washiriki na kukuza vipaji vyo, jumla washiriki wapo 42”.

Kumbuka kuwa jumuiya ya Skaut Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi katika Atabatu Abbasiyya, huandaa hema za kutoa mafunzo mbalimbali ya fani tofauti kwa wanachama wake kila mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: