Wanafunzi 120 kutoka chuo kikuu wapo katika wenyeji wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimepokea ugeni wa wanafunzi (120) kutoka chuo kikuu cha Kufa, chini ya utaratibu wa kupokea wanafunzi wa vyuo kupitia mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel.

Makamo rais wa kitengo tajwa Sayyid Muhammad Jalukhani Mussawi amesema “Atabatu Abbasiyya inaendelea kupokea wageni mbalimbali, wakiwemo wanafunzi wa chuo na shule za kisekula, ambao ratiba ya ziara yao huwa na vipengele vingi”.

Akaongeza kuwa: “Ratiba imeanza kwa kufanya ziara kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), sambamba na kutembelea sehemu mbalimbali za malalo hizo takatifu na kutambua huduma zinazotolewa kwa mazuwaru, kisha wakafanya kikao ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaendelea kuwema “Miongoni mwa mihadhara iliyotolewa upo wa lugha ya kiengereza, ulitolewa na Shekhe Khalidi Yaquut, akaeleza kuhusu harakati ya Imamu Hussein na malengo yake, na namna ilivyofanikiwa kubakia hai hadi sasa kwa sababu ililenga kumkomboa mwanaadamu na kutenda haki”.

Mwisho wa ziara hiyo wanafunzi wakatoa shukrani nyingi kwa Atabatu Abbasiyya na uongozi mkuu, ikiwemo idara ya uhusiano wa vyuo vikuu, wakaomba misafara kama hii iendelee kufanywa siku zijazo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: