Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu kimeandaa warsha kwa watumishi wa idara ya malezi katika mji wa Dhiqaar

Maoni katika picha
Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa warsha yenye anuani isemayo (Kuandaa malengo ya kimalezi) kwa kundi la walimu na wakuu wa shule katika idara ya malezi ya mkoa wa Dhiqaar.

Kiongozi wa idara ya mafunzo bwana Karaar Hussein Maamuri amesema: “Tunafanya warsha hizi kwa ajili ya kujenga uwezo wa washiriki wa kufikia malengo kwa njia za kielimu”.

Akaongeza kuwa “Mada mbalimbali zimefundishwa ikiwa ni pamoja na kutambua malengo ya kielimu na njia bora ya kuandaa malengo”.

Akasema “Warsha ilikua na mitihati mbalimbali” akabainisha kuwa “Warsha itadumu kwa muda wa siku tatu, kila siku watasoma saa tano, jumla kuna washiriki (40)”.

Kumbuka kuwa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendelea kuratibu warsha na semina za kielimu, zinazo lenga kujenga uwezo wa watumishi wa Ataba tukufu, pamoja na watumishi wa taasisi zingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: