Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya siku ya Jumamosi katika jengo la Alqami, imepokea makumi ya wanafunzi wanaopenda kujiunga na mradi wa kuhifadhi Qur’ani tukufu unaoendeshwa na idara ya tahfiidh katika mkoa wa Karbala.
Wanafunzi wengi wenye uwezo mzuri wa kusoma Qur’ani wamekuja kujisajili katika wiki hii.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu inaendesha mradi wa kuhifadhi Qur’ani katika mkoa mtukufu wa Karbala na mikoa mingine, pamoja na kuhifadhi Qur’ani wanafunzi hufundishwa masomo ya malezi, Akhlaqi, Hukumu za usomaji wa Qur’ani, Naghma, Sauti, bila kusahau vipindi vya michezo na safari za kidini.