Zaidi ya sahani 2000 za chakula zimetolewa na kitengo cha mgahawa kwa kikosi cha uokozi katika eneo la Stesheni.

Maoni katika picha
Kitengo cha mgahawa katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa zaidi ya sahani 2000 za chakula kwa kikosi cha uokozi na askari waliopo stesheni ndani ya siku tatu.

Makamo rais wa kitengo cha mgahawa bwana Alaa Abdulhussein amesema: “Kufuatia maelekezo ya uongozi mkuu wa Ataba tukufu, tumetoa zaidi ya sahani 2000 za chakula kwa kikosi cha uokozi na askari waliopo stesheni magharibi ya Karbala”, akaongeza kuwa “Kitengo cha mgahawa katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimezowea kutoa huduma ya chakula katika maeneo yanayo hitaji huduma hiyo na kwenye mazingira magumu”.

Akafafanua kuwa “Tambua kuwa tumefanya kazi kwa muda wa siku tatu mfululizo na bado tunaendelea”, Akasema “Tumegawa mamia ya chupa za maji safi ya kunywa kwa kikosi cha uokozi na kila aliyopo eneo hilo”.

Kumbuka kuwa stesheni ya Karbala ilibomoka siku ya Jumamosi na kufunika idadi kubwa ya watu chini ya vifusi, jambo ambalo limepelekea kikosi cha uokozi kuweka kambi hapo kwa shughuli za uokozi, hadi sasa wamefanikiwa kuokoa watu wengi, na kazi bado inaendelea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: