Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki kwenye maonyesho ya Taratiili-Sajadiyya awamu ya nane

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha Habari na utamaduni na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, imeshiriki kwenye maonyesho ya (Taratiili-Sajadiyya) yanayo simamiwa na Atabatu Husseiniyya awamu ya nane katika mkoa wa Karbala.

Kiongozi wa idara ya maonyesho katika kitengo cha Habari na utamaduni Sayyid Muhammad Aaraji amesema: “Kitengo cha Habari na utamaduni kimeshiriki kikiwa na machapisho (350) yanayo jumuisha majarida, vitabu vya Dini na Aqida”, akaongeza kuwa “Machapisho yote tuliyonayo yamechapishwa na Darul-Kafeel”.

Akaendelea kusema: “Vitabu vikuu vinavyo onyeshwa kwenye maonyesho haya ni Mausua ya fatwa takatifu ya kujilinda na Mausua zingine za kidini” akasema kuwa “Kituo cha tafiti za kiislamu kimeshiriki pia kikwa na machapisho yake Madhubuti”.

Kiongozi wa idara ya ufuatiliaji na mawasiliano katika kitengo cha maarifa ya Sayyid Alaa Hamdi Matwaru amesema “Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kimeshiriki kikiwa na zaidi ya anuani (150) vikiwemo vitabu maalum vya utamaduni, historia, na vitabu vya uhakiki wa historia ya mji wa Karbala na miji mingine”.

Tambua kuwa baadhi ya nakala za Taratili-Sajadiyya zinaonyeshwa kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu kuanzia tarehe 20 hadi 30 mwezi huu wa nane, kuna zaidi ya taasisi za uchapaji na usambazaji (60) za kitaifa na kimataifa zinazoshiriki.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imeshashiriki kwenye maonyesho mengi ya aina hiyo, kitaifa na kimataifa kwa lengo la kusambaza fikra ya uislamu asili, sambamba na kuonyesha vitabu vya elimu mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: